BONGO AFYA: ALOE VERA NA MAJI YA MOTO HUTIBU MAPELE YA NDEVU.

Japokuwa kiafya ni tatizo dogo,mapele yanayotokea baada ya kunyoa ndevu au nywele za kwapani na sehemu nyingine,husababisha muhusika kukosa raha,kujikuna na kushindwa kujiamini hasa anapokuwa mbele za watu.
Wengine hulazimika kutimia krimu Kali kwa lengo la kuondoa mapele hayo,japokua haishauriwi sana kutumia krimu hizo kwani zina madhara kwa ngozi.
Leo nataka tujadiliane kuhusu mbinu nyepesi za kumaliza tatizo hili.

Mahitaji:
•Aloevera
•Maji ya moto
•Kitambaa
Chukua jani bichi la aloevera,likate na utoe mibamiba ya pembeni,kisha lipasue katikati kupata ute wake,chukua ute huo na uupake sehemu uliyonyoanywele,muda mfupi baada ya kunyoa.Uache ute huo mpaka ukauke kabisa
  kisha baada ya hapo,safisha kwa maji mengi masafi.
Kama umeshindwa kupata jani halisi la aloevera,unaweza kutumiajuisi ya aloevera ambayo inauzwa madukani.Ipake juisi ya aloevera eneo ulilonyoa na uache mpaka ikauke.
Baada ya hapo safisha kwa maji mengi masafi.
Njia nyingine,unaweza kutumia maji ya moto kuzuia mapele hayo. Namna ya kufanya,ukishamaliza kunyoa chukua taulo dogo au kitambaa na ukiloweshe kwenye maji ya moto,toa kisha kikandamize kitambaa hicho kwenye eneo ulilonyoa na shikilia mpaka joto la maji lipungue,rudia tena kwa zaidi ya dakika tano.
Hakikisha unaendelea na zoezi hilo Mara Kwa Mara ,hata kama hujatoka kunyoa.

Post a Comment

0 Comments