MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI ATEKWA NA WATU WASIOJULIKANA.

TAARIFA ZA AWALI: Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6
-
Inadaiwa usiku huo Nondo ali-“left” makundi yake yote ya WhatsApp, jambo lililozua taharuki. Hata alipopigiwa simu, hakupokea
-
Aidha, Nondo anadaiwa kutuma ujumbe(SMS) kwa rafiki yake kuwa "I AM AT HIGH RISK" na baada ya hapo hajapatikana tena hewani hadi sasa
-
Taarifa kutoka kwa Afisa Habari wa Mtandao wa Wanafunzi, zinasema ni kweli hajulikani yuko wapi mpaka sasa, hata Walezi wake(Mama na Baba yake mdogo) hawajui yuko wapi
-
Viongozi wa Mtandao wa Wanafunzi wamefika Kituo cha Polisi kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwaajili ya kutoa taarifa za kupotea kwake .

Post a Comment

0 Comments