BARAKAH DA PRINCE AMERUDI NA HII 'NIMEKOMA' BAADA YA KIMYA KIREFU

Baada ya kimya kirefu kwa takribani mwaka mmoja, Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince ametangaza kuachia wimbo wake wa kwanza ‘NIMEKOMA’ kwa mwaka 2020.

Akizungumzia wimbo huo, Barakah The Prince amesema kuwa ni wimbo ambao ameutunga kwa hisia kali na unatoka leo, Ukiwa umeandaliwa na Producer, Dee Classic.

Kwa upande mwingine, Barakah The Prince ameeleza sababu za kukaa kimya kwenye muziki kwa takribani mwaka mmoja, Na kudai kuwa alikuwa chimbo akiandaa Album yake ya kwanza na mambo ya kifamilia.
“Nimerudi rasmi kwenye gemu baada ya kukaa kimya bila kutoa ngoma mwaka 2019. Unajua kimya kingi kina mshindo, Nilijichimbia kuandaa kazi zenye viwango, Na naahidi ujio wangu wa ngoma ya ‘NIMEKOMA’ utakuwa ni mwanzo tu kwani nina ngoma kibao ambazo zitatoka mwaka huu, Na zitakuwa pia kwenye Album yangu ambazo zitatoka mwaka huu Mungu akipenda,” amesema Barakah.
Mkali huyo aliyewahi kutamba na ngoma kama Acha Niende, Amesema kuwa Audio ya wimbo wa ‘NIMEKOMA’ inatoka Leo Alhamisi 12, 03, 2020 na video itatoka wikiendi hii ikiwa imeongozwa na Director, Hanscana.

Post a Comment

0 Comments