FAHAMU ZAIDI:JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA

Virusi vya Corona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ni kundi la virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa kwa wanyama(mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu[1]. Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.

Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu. Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wabaya kukuvamia na kusababisha maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua(influenza), yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari kama nimonia inayoweza kusababisha kifo. Hivyo inatakiwa watu wapunguze kutumia kwa pamoja vitu hatarishi kama vile vya ncha kali[4].
Hadi sasa hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyajihutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.
Aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ulikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.
Maambukizi husambaa hasa kwa majimaji ya mwilini, kama matone madogo ya mate au chafya; mtu aliyeambukizwa atakuwa na virusi kwenye mikono yake akigusa pua au mdomo. Inawezekana mtu aliyeambukizwa asionyeshe dalili za ugonjwa bado lakini anaweza kupitisha virusi tayari.
Unashauriwa:
  • kunawa mikono mara kwa mara kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
  • usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
  • epuka kuwa karibu sana na wagonjwa, tumia barakoa ya kinga ukimhudumia mgonjwa
  • ikiwezekana epuka kuingia katika msongamano mkubwa wa watu maana wenye virusi hawaonekani kirahisi.
  • kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga yako ni dhaifu katika hali hii)
  • tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya choo / toilet paper) uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
  • safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombemezadawatisimu yako)[16]
  • Source:Wikipedia,written by Capital Ado

  • Thanks4beingwith Us.

Post a Comment

0 Comments